Leviticus 24:2-4

2 a“Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima. 3 bNje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Haruni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 4 cTaa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima.

Copyright information for SwhKC